Praia,Cape Verde.
UGANDA sasa ndiyo vinara wa kundi L ambalo pia timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars imo hii ni baada ya jana Jumapili Usiku ikiwa ugenini kuwafunga wenyeji wao Cape Verde kwa bao 1-0 huko Praia katika mchezo mkali wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2019 nchini Cameroon.
Bao lililoipa Uganda pointi zote tatu ugenini limefungwa katika dakika ya 83 na mshambiliaji wa KCCA Geoffrey Sserunkuma.
Sserunkuma aliyekuwa ameingia uwanjani dakika chache kuchukua nafasi ya Emmanuel Okwi aliyekuwa na kadi ya njano alifunga bao hilo muhimu akimalizia krosi safi toka wingi ya kushoto iliyopigwa na Derrick Nsibambi aliyekuwa amegongeana vyema na Khalid Aucho.
Ushindi huo umeifanya Uganda ichupe mpaka kileleni mwa kundi L baada ya kufikisha pointi tatu na kuzishusha Lesotho na Tanzania katika nafasi za pili na tatu baada ya juzi Jumamosi kufungana bao 1-1.
Uganda iliwakilishwa na: Denis Onyango (GK) (C), Nicholas Wadada, Godfrey Walusimbi, Bernard Muwanga, Murushid Jjuuko, Hassan Wasswa,Khalid Aucho, Faruku Miya,Emmanuel Okwi,Derrick Nsibambi na Isaac Muleme.
0 comments:
Post a Comment