Dar Es Salaam,Tanzania.
Baada ya kufutwa utaratibu wa
mawakala ‘agents’ wa wachezaji wa
kulipwa, Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA), lilitangaza utaratibu
mpya wa kukasimu majukumu hayo
kwenye ngazi ya mashirikisho kwa kila
taifa.
Hivyo kwa mwaka 2016/2017, hakuna
usajili wala uhamisho uliofanywa na
watu wa kati yaani intermediaries
wanaotambulika na TFF.
TFF - Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania, linakwenda sambamba na
utaratibu huo wa mabadiliko na kwa
sasa linakamilisha mipango ya kusajili
watu wa kati wa usajili watakaofahamika
kama intermediaries.
Usahili wa kati utatangazwa baada ya
kikao cha Kamati ya Utendaji
kitakachojadili kanuni za watu wa kati
hapo baadaye.
0 comments:
Post a Comment