728x90 AdSpace

Wednesday, June 14, 2017

Yanga SC yaanza usajili rasmi,yamnasa beki wa Jang'ombe



Dar Es Salaam,Tanzania.

Mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara ,Yanga SC wameanza kukiimarisha kikosi chao tayari kwa michuano mbalimbali msimu ujao baada ya leo kumsajili beki kisiki wa kati wa timu ya Taifa ya Jang'ombe, Abdallah Haji Shaibu maarufu kama "Ninja".

Ninja amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuwatumikia mabingwa hao ambao katika kipindi cha hivi karibuni wamekuwa kimya sana katika masuala mazima ya usajili kiasi cha kuanza kubezwa kuwa wamefulia.



  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Yanga SC yaanza usajili rasmi,yamnasa beki wa Jang'ombe Rating: 5 Reviewed By: Unknown