Glasgow,Scotland.
KIPA wa Scotland,Cammy Bell, ameingia katika vitabu vya kumbukumbu za dunia baada ya jana Jumamosi kudaka penati tatu ndani ya dakika 23 za kipindi cha kwanza na kuiwezesha timu yake ya Dundee United kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Dunfermline katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Scotland uliochezwa katika uwanja wa East End Park.
Bell,30,aliyewahi pia kuzichezea timu za Rangers na Kilmarnock alidaka penati hizo dakika za 1,28 na 33 zilizopigwa na Gavin Reilly,Nicky Clark na Paul McMullan.
Ikumbukwe wapo makipa waliowahi kudaka penati tatu katika mchezo mmoja wa soka lakini linapokuja suala la kudaka penati tatu katika kipindi kimoja cha mchezo yaani ndani ya dakika 45,Bell,ameweka rekodi ya peke yake.
Mabao ya Dundee United katika mchezo huo yalifungwa na Simon Murray na Tony Andreu aliyefunga mabao mawili. Bao la Dunfermline limefungwa na Michael Paton.
0 comments:
Post a Comment