Cairo,Misri.
SHIRIKISHO la soka Afrika,CAF,limesema kuwa michuano ya soka kwa nchini za ukanda wa Afrika ,AFCON,itafanyika nchini Gaban kama ilivyopangwa hapo awali licha ya nchi hiyo kwasasa kuwa katika mgogoro mkubwa wa kisiasa uliosababishwa na kuchaguliwa kwa mara nyingine kwa Rais wa nchi hiyo Ali Bongo.
CAF kupitia kwa msemaji wake,Junior Binyam,imesema kwa sasa hakuna mabadiliko yoyote yaliyofikiwa juu ya kuipokonya uwenyeji Gabon lakini ameonya kuwa kunaweza kukatokea mabadiliko ikiwa hali ya usalama itazidi kuwa mbaya nchini humo.
Wakati huohuo Binyam ameongeza kuwa kati ya Septemba 21-27 CAF itakuwa na kikao chake cha kawaida na moja kati ya ajenda zitakazojadiliwa ni kuhusu suala la mgogoro wa kisiasa nchini Gabon.
Droo ya upangaji wa makundi ya fainali za AFCON itafanyika Octoba 19 mwaka huu huko Libreville na michuano itaanza kutimua vumbi lake Januari 14 na kufikia tamati Februari 5,2017.
0 comments:
Post a Comment