728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 05, 2016

    OWEN AFICHUA KILICHOFANYA ASHINDWE KUMALIZIA SOKA YAKE LIVERPOOL


    Liverpool,Uingereza.

    KAMA kuna kitu ambacho kinachousononesha na kuumiza sana moyo wa Mshambuliaji wa zamani wa England,Michael Owen, basi ni kushindwa kumalizia soka yake katika klabu yake kipenzi ya Liverpool.

    Katika kitabu chake kipya kinachoitwa Ring of Fire,Owen,amefichua kwamba alitamani kurejea Liverpool tangu siku ya kwanza alipoondoka Anfield na kujiunga na Real Madrid mwaka 2004 kwa ada ya £8m lakini bahati mbaya na kuringiwa ndiko kulikomkwamisha.

    Amesema "Kila nilipokuwa napatikana,Liverpool ilikuwa na washambuliaji wengi.Na kila Liverpool iliponihitaji,nilikuwa majeruhi.Mwisho sikuwa yule mchezaji niliyewahi kuwa hapo kabla,sikuhitajika tena.Sikuwa bora tena machoni pao.

    Ameendelea kusema "Katika kila hatua - Kila majira ya joto,nilikuwa nikimpigia simu Carra (Jamie Carragher) na kumwambia atafute njia ya kuongea na Rafa Benitez wakati mwingine Kenny Daglish na Brendan Rodgers ili niweze kurudi Liverpool.Nilitaka kuweka mambo sawa.

    Nilipogundua kuwa Liverpool haiitaji kufanya dili na mimi niliongea na Kocha wa Manchester United (Alex) Ferguson kwa mara nyingine.Akaonyesha kunihitaji,nilikuwa na miaka 29 wakati huo je nilipaswa kustaafu kisa Liverpool hawakunihitaji?Hapana.

    Owen aliihama Liverpool mwaka 2004 akiwa ameifungia mabao zaidi ta 150 na kujiunga na Real Madrid lakini baada ya msimu mmoja alijikuta akitua Newcastle United baada ya maisha ya Hispania kumwendea kombo.Aliitumikia Newcastle United kuanzia mwaka 2005-09 kisha akajiunga na Manchester United na kumalizia soka yake Stoke City mwaka 2012.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OWEN AFICHUA KILICHOFANYA ASHINDWE KUMALIZIA SOKA YAKE LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top