728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 02, 2016

    MAKOCHA,WACHEZAJI WANAOWANIA TUZO YA MWEZI AGOSTI EPL HAWA HAPA

    London, Uingereza.

    CHAMA cha soka nchini England FA leo mchana kimetoa orodha ya Makocha/Mameneja na Wachezaji walioingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya Makocha na Wachezaji waliofanya vizuri Mwezi Agosti.

    Makocha Jose Mourinho (Manchester United),Pep Guardiola (Manchester City) Antonio Conte (Chelsea) na Mike Phelan (Hull City) wameteuliwa kuwania tuzo ya Meneja bora wa Mwezi (Manager of the Month award) kutokana na kuwa na mwanzo mzuri.

    Jose Mourinho,Pep Guardiola na Antonio Conte wameingia katika mchuano huo baada ya kuviongoza vikosi vyao kushinda michezo mitatu ya mwanzo ya ligi kuu England.Mike Phelan ameingia katika mchuano huo baada ya kuiongoza Hull City kushinda michezo yake miwili ya mwanzo licha ya kuwa na kikosi kilichokuwa na wachezaji 13 pekee waliokuwa fiti.

    Nyota wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti maarufu kama Player of the Month award ni Raheem Sterling (Manchester City), Eden Hazard (Chelsea),Antonio Valencia (Manchester United) na Curtis Davies (Hull City)

    Washindi wa tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwezi watatangazwa Septemba 6,2016

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAKOCHA,WACHEZAJI WANAOWANIA TUZO YA MWEZI AGOSTI EPL HAWA HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top