Dar Es Salaam,Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye
ametoa ofa kwa wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016 katika
mchezo wa mpira wa miguu utakaozikutanisha timu za vijana taifa za
Tanzania na Congo-Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe,
jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya
miaka. Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na
timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa
fainali hizo.
Nape alitoa ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi
Septemba alipata kifungua kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako
alitoa Sh 200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti
Serengeti Boys ambao walichangia Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka
kwa wadau wengine.
Nape ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha
hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake
itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa
fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo
mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”
Kuingia bure kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal
Malinzi amemshukuru Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo
imelenga kutoa hamasa kwa Watanzania kwenda kushangilia timu yao.
Katika mchezo
huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema kwamba amemaliza kila
kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani leo kuishangilia timu
yao, utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako mpiga kipenga atakuwa
Nelson Fred akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie wakati
mwamuzi wa akiba akiwa Allister Barra. Kamishna wa mchezo atakuwa
Gladmore Muzambi kutoka Zimbawe.
0 comments:
Post a Comment