Leon,Hispania.
HISPANIA imeishikisha adabu timu kibonde ya Liechtenstein baada ya usiku huu kuichapa mabao 8-0 huko Estadio Reino de Leon katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi kwa ukanda wa nchi za Ulaya.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi Simon Lee Evans kutoka Wales,imeshuhudiwa Hispania ikijipatia mabao yake kupitia kwa Diego Costa (10', 67'),Sergi Roberto (55'),David Silva (59', 91'),Vitolo (60') na Alvaro Morata (82', 83')
Katika mchezo mwingine wa kufuzu kombe la dunia Italia ikiwa ugenini nayo imechomoza na ushindi mnono baada ya kuwachapa wenyeji wao Israel kwa jumla ya mabao 3-1.
Mabao ya Italia yamefungwa na Graziano Pellè 14',Antonio Candreva 31' na Ciro Immobile 83' huku lile la kufutia machozi la Israel likifungwa na Tal Ben Haim 35'.
Matokeo Mengine
0 comments:
Post a Comment