Swansea,Wales.
CHELSEA imeshikwa shati na Swansea City baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliochezwa katika uwanja wa Liberty,Wales.
Chelsea ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Diego Costa kufunga kwa mkwaju mkali dakika ya 18 akiunganisha pasi ya Oscar Dos Santos.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza na kuifanya Chelsea iende mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo moja.
Katika kipindi cha pili Swansea City ilionekana kuchangamka tofauti na kipindi cha kwanza kwani dakika ya 59 Gylfi Sigurdsson aliifungia bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati lililofuatiwa na bao la pili lililofungwa dakika ya 62 na Leroy Fer ambaye alikuwa mwiba mkali kwa walinzi wa Chelsea.
Diego Costa kwa mara nyingine aliirudisha Chelsea mchezoni baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 81 ya mchezo kwa tiki taka na kufanya mchezo uishe kwa sare ya mabao 2-2.
0 comments:
Post a Comment