Dar Es Salaam,Tanzania.
SIMBA SC imeutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Uhuru baada ya jioni ya leo kuichapa Mtibwa Sugar ya Manungu kwa mabao 2-0 katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mabao ya Simba SC katika mchezo wa leo yamefungwa na Ibrahim Ajib kwa kichwa dakika ya 53 akiunganisha kona ya Shiza Kichuya.
Bao la pili limefungwa na Mrundi Laudit Mavugo dakika ya 67 baada ya kumegewa pande safi na Mwinyi Kazimoto.
Matokeo hayo yameifanya Simba SC ifikishe pointi 10 baada ya kucheza michezo minne.
0 comments:
Post a Comment