London, England.
MSHAMBULIAJI wa Nottingham Forest,Mdenmark Nicklas Bendtner,amesema atashangalia ikiwa atafunga bao dhidi ya timu yake ya zamani ya Arsenal katika mchezo wao wa leo Jumanne usiku wa michuano ya kombe la ligi maarufu kama EFL
Bendtner,28,ambaye hivi karibuni alijiunga na Nottingham Forest kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kutemwa na VFL Wolfsburg ya Ujerumani ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari ambao walitaka kujua kama atashangilia ikiwa atafunga bao dhidi ya Arsenal iliyomlea na kumpa jina.
Bila kupepesa macho wala kuuma uma maneno ,Bendtner,amekiri kuwa atashangilia lakini si kwa kiwango kikubwa kwani anaiheshimu Arsenal na anaipenda Arsenal.
Bendtner aliichezea Arsenal kati ya mwaka 2005 na 2014 ambapo alifanikiwa kucheza michezo 171 kabla ya kutemwa na kujiunga na VFL Wolfsburg ambayo pia ilimtema mwishoni mwa msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment