Jinja,Uganda.
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara,Kilimanjaro Queens,leo jioni itajitupa katika uwanja wa Fufa Technical Centre huko Jinja kuvaana na timu ya taifa ya wanawake ya Kenya,Harambee Starlets katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa utakuwa ni mgumu na wenye kusisimua, utatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na wa nne kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia.
Kilimanjaro Queens imefuzu fainali baada ya kuwachapa wenyeji Uganda katika mchezo wa nusu fainali huku Harambee Starlets ambao ni tishio katika michuano hiyo wakiing'oa Ethiopia.
Akiongea na waandishi wa kuelekea mchezo wa fainali,Katibu Mkuu wa CECAFA,Nicholas Musonye,amesema michuano ya mwaka huu haitakuwa na zawadi za fedha kwa timu zilizofanya vizuri wala wachezaji bora kutokana na michuano hiyo kukosa wadhamini.
Musonye ameahidi kuwa katika michuano ijayo CECAFA itakuwa imepata udhamini na timu shiriki zitegemee mabadiliko makubwa hasa katika zawadi za fedha.
Hii ni mara ya pili kwa michuano ya CECAFA kwa wanawake kufanyika.Mara ya kwanza michuano hiyo kufanyika ilikuwa mwaka 1986 na Zanzibar kuibuka mabingwa.
0 comments:
Post a Comment