728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 07, 2017

    Arda Turan astaafu soka la kimataifa baada ya kutembeza ubabe kwa Mzee wa miaka 70


    Istanbul,Uturuki.

    KIUNGO wa Barcelona Arda Turan amestaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Uturuki.

    Turan mwenye umri wa miaka 30 ametumia ukurasa wake wa instagram kutangaza uwamuzi huo zikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu afukuzwe kwenye kambi ya Uturiki na kocha Fatih Terim.

    Juzi Jumatatu Turan alifukuzwa kambini baada ya kugombana na mwandishi wa habari wa gazeti la michezo la Milliyet,Bilal Mese wakiwa ndani ya ndege wakitokea Macedonia walikokwenda kucheza mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya bila kufungana.

    Ndege ikiwa angani Turan alimvamia Mese na kumkaba koo lake na kumtolea lugha kali akidai kuwa mwandishi huyo mwenye miaka 70 alimtukana wakati wa fainali za Euro zilizofanyika mwaka jana nchini Ufaransa.

    Turan ambaye alikuwa ni nahodha amevituhumu vyombo vya habari vya Uturuki kuwa vimekuwa vikimuandika vibaya.Vimekuwa vikiingilia maisha binafsi ya watu na kuandika habari za uzushi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Arda Turan astaafu soka la kimataifa baada ya kutembeza ubabe kwa Mzee wa miaka 70 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top