Dar Es Salaam,Tanzania.
Simba imeomba kurudi kutumia Uwanja wa Taifa kama ilivyokuwa awali badala ya kuendelea kuutumia Uwanja wa Uhuru kwa michezo yake ya ligi kuu bara.
Tayari Simba kupitia Katibu Mkuu wake,Patrick Kahemele imetuma barua kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na kuomba kurudi kutumia Uwanja wa Taifa huku sababu ya kutaka kurudi kutumia Uwanja wa Taifa kuwa ni hofu ya usalama wa afya ya wachezaji wake kutokana na plastiki zinazoshika nyasi katika uwanja wa Uhuru.
Sababu nyingine ambayo imeelezwa na Simba ni uwanja kuwa mdogo, ikitolea mfano mchezo wa Azam ambao ulipigwa Jumamosi kwa baadhi ya mashabiki wake kushindwa kuingia kutokana na udogo wa uwanja.
Aidha Simba imetoa ushauri kwa TPLB kuwa uwanja wa Uhuru uwekewe plastiki mpya ili kuondoa hofu ya wachezaji wake kupata majeruhi na kama wataruhusiwa kuchezea uwanja wa Taifa basi waanze kuujaribu mfumo wa kieletroniki kabla ya mchezo wa Oktoba mosi ambao watapambana na Yanga.
0 comments:
Post a Comment