Dar Es Salaam,Tanzania.
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) imeendelea tena leo kwa michezo mitatu kupigwa katika mikoa ya Mtwara,Dar Es Salaam na Mbeya.
Dar Es Salaam:Simba SC ikiwa katika uwanja wa Uhuru,Dar Es Salaam,imeifunga Ruvu Shooting Stars mabao 2-1.Mabao ya Simba SC yamefungwa na Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo huku lile la Ruvu likifungwa na Abrahman Musa.Dakika ya 79 Jabir Aziz wa Ruvu alionyeshwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Mtwara:Ndanda FC ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona imetoka sare ya bila kufungana na Yanga SC.
Mbeya:Tanzania Prisons ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa kumbukumbu ya Sokoine imefungwa bao 1-0 na Azam FC.Bao limefungwa na Kipre Balou.
0 comments:
Post a Comment