Genk,Ubelgiji.
Kara Mbodji (Pichani) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia RSC Anderlecht bao la kwanza na kuiwezesha kuitwanga KRC Genk ya Mtanzania,Mbwana Samatta,kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Ubelgiji ulioisha hivi punde katika uwanja wa Cristal Arena,Genk.
Bao la pili la RSC Anderlecht limefungwa na Hamdi Harbaoui.Katika mchezo huo wenyeji Genk walilazimika kumaliza pungufu baada ya wachezaji wao wawili kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Samatta hakucheza mchezo wa Leo kutokana na kuwa majeruhi.
0 comments:
Post a Comment