728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, September 10, 2016

    MH NAPE KUZURU TFF LEO JUMAMOSI, KUTETA NA MALINZI

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) leo Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

    Akiwa TFF kuanzia saa 4.30 asubuhi, Waziri Nape atazungumza na Mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na Sekretarieti kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ambao TFF imeawaalika katika ziara hiyo.

    Katika ratiba hiyo, Nape ataonyeshwa maendeleo ya michezo hususani mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya Airtel na kuratibiwa na TFF ambako kwa mikoa mbalimbali iliyofanya vema, leo timu za wanawake na wanaume zitacheza hatua ya nusu fainali kabla ya fainali za Jumapili ambazo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MH NAPE KUZURU TFF LEO JUMAMOSI, KUTETA NA MALINZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top