Accra,Ghana.
NAHODHA msaidizi wa timu ya Taifa ya Ghana,Andre Ayew,ameshauriwa kutumia tiba asili (Miti Shamba) ili kuondokana na majeraha aliyonayo.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama Cha Soka cha Ghana,Francis Akenten,wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Nhyira FM.
"Kuna wataalamu wengi wa tiba za asili hapa Ghana ambao wanaweza kutibu majeraha ya Andre Ayew kwa muda wa wiki mbili tu na akapona vizuri kabisa.Nitaongea na baba yake kuhusu hilo".Alinukuliwa Akenten
Akenten ametoa ushauri huo kwa kile anachoamini kuwa kutokuwepo kwa Ayew kutaathiri maandalizi ya timu ya taifa ya Ghana katika michuano ijayo ya AFCON itakayofanyika nchini Gabon Januari mwakani.
Kwa sasa Ayew yuko nje ya dimba kwa kipindi cha miezi minne akiuguza jeraha la paja alilolipata wakati akiitumikia klabu yake mpya ya Westham United katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu England ulioisha kwa klabu hiyo kufungwa mabao 2-1 na Chelsea.
0 comments:
Post a Comment