728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 12, 2017

    USAJILI:AC Milan yaipora Arsenal mshambuliaji


    Milan,Italia.

    AC MILAN imefanya kile ambacho Azam FC imefanya kwa Yanga katika siku za hivi karibuni imeipora Arsenal mshambuliaji mahiri wa FC Porto,Andre Silva na kumsajili kwa ada ya £35m.

    Silva mwenye umri wa miaka 21 aliwasili jijini Milan leo asubuhi na kuanza kufanyiwa uchunguzi wa afya yake kabla ya jioni hii kuingia mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia miamba hiyo ya Seria A.

    Mara kadhaa msimu huu Silva alikuwa alihusishwa kutakiwa na Arsenal hasa baada ya kufunga mabao 24 kwenye ligi kuu ya soka nchini Ureno lakini amejikuta akitua AC Milan baada ya Arsenal kushindwa kufikia bei yake.

    Silva anakuwa mchezaji wanne kujiunga na AC Milan katika siku za hivi karibuni. Wengine ni Mateo Musacchio, Ricardo Rodriguez na Franck Kessie.Mpaka sasa AC Milan imetumia jumla ya €100m kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake ambacho kimekuwa hakifanyi vizuri katika miaka ya karibuni.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:AC Milan yaipora Arsenal mshambuliaji Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top