728x90 AdSpace

Monday, June 12, 2017

Taifa Stars kambini tena Juni 14 kujiwinda na Cosafa


Dar Es Salaam,Tanzania.

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, itaingia kambini tena Juni 14, mwaka huu kujiandaa na michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka la Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu ambako Taifa Stars itakwenda Misri, Juni 20, mwaka huu.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amepanga kufanya mabadiliko madogo ya kikosi cha Taifa Stars kitakaochokwenda kushiriki michuano hiyo.

Kocha kesho atafanya uteuzi wa wachezaji wengine atakaowajumuisha kwenye kikosi chake, atafanya mabadiliko kidogo hivyo  kesho atatangaza majina ya wachezaji ambao wataingia kambini kujiandaa na michuano hii ya Cosafa inayoanza Juni 25 huko Afrika Kusini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Taifa Stars kambini tena Juni 14 kujiwinda na Cosafa Rating: 5 Reviewed By: Unknown