728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, September 03, 2016

    HAMISI KIIZA DIEGO ATAMBULISHWA RASMI KUWA MALI YA FREE STATE STARS


    Bethlehem,Afrika Kusini.

    Klabu ya Free State Stars iliyokuwa ikichezewa na Mtanzania Mrisho Halfani Ngassa "Anko" Jana Ijumaa ilitambulisha nyota wake wapya iliyowasajili kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Afrika Kusini maarufu kama ABSA Premiership.

    Kati ya nyota waliotambulishwa hiyo jana alikuwemo pia Mshambuliaji Hamisi Kiiza Diego aliyetemwa na Simba SC mwishoni mwa msimu uliopita kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mtovu wa nidhamu.

    Kiiza amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia miamba hiyo inayofahamika kwa jina lake la utani la Ea Lla Koto baada ya kufuzu majaribio ya wiki mbili.

    Mbali ya Kiiza,Free State Stars pia imewatambulisha nyota wake wengine wapya kama Mlinda Mlango Thela Ngobeni,Winga Ella Ken Armand pamoja na beki wa Kenya,Joseph Okumu.

    Kiiza anakuwa mchezaji wa tano kutoka nchini Uganda kujiunga na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.Wengine ni Dennis Onyango (Mamelodi Sundowns),Geoffrey Massa (Baroka), Aucho Khalid (Baroka), Boban Zirintunsa (Polokwane City) na Kirizsetom Ntambi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HAMISI KIIZA DIEGO ATAMBULISHWA RASMI KUWA MALI YA FREE STATE STARS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top