728x90 AdSpace

Friday, September 09, 2016

WAWILI KUCHUKUA NAFASI YA MKONGWE JOHN TERRY CHELSEA


                                                                             Ben Gibson

London,Uingereza.

CHELSEA imeanza mapema kujiandaa na maisha bila ya beki na nahodha wake,John Terry,35,hii ni baada ya kuripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kuwasajili mabeki wawili wazaliwa wa Uingereza.

Taarifa kutoka katika gazeti la The Daily Mail la leo Ijumaa zinasema meneja wa klabu hiyo,Antonio Conte,amewageukia mabeki Ben Gibson wa Middlesbrough na Michael Keane wa Burnley ili kuchukua nafasi ya Terry atakayeachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu.

                                                                         Michael Keane

Chelsea imeamua kuwatupia macho mabeki hao Waingereza ili kwenda sambamba na sheria za ligi kuu Uingereza ambazo zinaagiza vilabu kuwa na idadi kubwa za wachezaji wazawa katika vikosi vyao.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: WAWILI KUCHUKUA NAFASI YA MKONGWE JOHN TERRY CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown