728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 06, 2016

    MESSI ABAINISHA SABABU YA KUBADILI RANGI YA NYWELE ZAKE

    Buenos Aires,Argentina.

    STAA wa Barcelona na Argentina,Lionel Messi, amefichua sababu iliyofanya abadili rangi ya nywele zake kutoka nyeusi iliyozoeleka na kuwa nyeupe mfano wa pamba ya kutengenezea nguo.

    Messi,28,amemwambia mwigizaji nyota wa Argentina anayeitwa Mingo kuwa matukio ya ndani na nje ya uwanja [Kesi ya kukwepa kulipa kodi,Kufungwa na Chile] ndiyo yaliyofanya abadili rangi ya nywele zake na kusisitiza kuwa mabadiliko ya nywele zake ni sehemu ya kuonyesha kwamba ameanza upya.

    "Nimefanya mabadiliko na ninaanza kuanzia sifuri.Mengi yameendelea,mambo yametokea na nikajiambia natakiwa kuachana na yote na kuanza upya.

    Hivi karibuni Messi aligonga vichwa vya habari duniani baada ya kubadili rangi ya nywele zake ikiwa ni siku chate tu tangu atangaze kustaafu kuichezea Argentina kufuatia kufungwa na Chile katika mchezo wa fainali wa michuano ya Copa America Centenario.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MESSI ABAINISHA SABABU YA KUBADILI RANGI YA NYWELE ZAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top