London,England.
HATIMAYE Manchester City imepoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu England ikiwa chini ya kocha wake mpya,Pep Guardiola,baada ya jioni ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham Hotspurs katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa katika uwanja wa White Hart Lane,jijini London.
Tottenham Hotspurs imepata mabao yake dakika za 9 na 37 kupitia kwa Alexander Koralov aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa krosi ya Danny Rose.Bao la pili limefungwa na Delle Alli.akimalizia pasi safi ya Mkorea,Son Heung Ming,aliyekuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Manchester City.
0 comments:
Post a Comment