728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 03, 2015

    INTERPOL YATAKA MAAFISA WA FIFA WAKAMATWE

    Shirika la maafisa wa polisi wa kimataifa Interpol limetoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.

    Agizo hilo linawalenga maafisa
    wanne wa mashirika makuu pamoja na maafisa wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo aliyekuwa makamu wa raisi wa shirikisho hilo Jack Warner.

    Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita.

    Ilani hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe ,lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: INTERPOL YATAKA MAAFISA WA FIFA WAKAMATWE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top