728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 03, 2015

    BENITEZ NDIYE KOCHA MPYA MADRID

    Aliyekuwa kocha wa Napoli Rafa Benitez amethibitishwa kuwa kocha wa Real Madrid katika kandarasi ya miaka mitatu.
    Benitez mwenye umri wa miaka 55 anachukua mahala pake
    Carlo Ancelotti ambaye aliondoka katika kilabu hiyo miezi 12 tu baada ya kuisaidia kushinda kombe lao la kumi la vilabu bingwa Ulaya.
    Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa Napoli ,baada kufanikiwa na vilabu kadhaa vya Ulaya.

    Baada ya kuisaidia Valencia kushinda kombe la Uefa mwaka 2004,mwaka unaofuatia alielekea Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside.

    Miaka miwili baadaye aliisaidia Liverpool kufika katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa Chelsea waliposhinda kombe la Yuropa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BENITEZ NDIYE KOCHA MPYA MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top