Dar es salaam,Tanzania.
Yanga imempa nafasi ya mwisho straika wake, Hussein Javu ambaye alikuwa kwenye mkumbo wa kutemwa na kuamua kumbakiza kwa ajili ya msimu ujao.
Javu alikuwa kwenye rundo la wachezaji zaidi
ya saba ambao wataonyeshwa mlango wa kutokea Jangwani, lakini ghafla akanusurika ikiwa ni nafasi ya mwisho kuhakikisha anaonyesha kiwango kizuri kwenye upinzani mbele ya Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Kpah Sherman ambaye hatima yake bado ipo shakani.

Uhakika kutoka ndani ya kamati nyeti klabuni hapo ni kwamba Javu amepewa nafasi ya upendeleo kuendelea kuwemo kikosini msimu ujao, huku Tegete akipewa mkono wa kwa heri baada ya kukaa kikosini hapo zaidi ya misimu miwili bila mafanikio.
“Javu atakuwepo, tumeamua kumpa nafasi tena ili akasaidie katika safu ya ushambuliaji, lakini kwa Tegete hapana, tumemuacha aangalie maslahi kwingine,” kilisema chanzo hicho.
Baadhi ya nyota wanaotajwa kutemwa ni Jerry Tegete, Rajab Zahir, Nizar Khalfan, Alphonce Matogo, Hassan Dilunga na Hamis Thabit ambaye alikuwa kwa mkopo Stand United.
0 comments:
Post a Comment