Leverkusen,Ujerumani.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anaichezea Bayer Leverkusen,Javier Hernández maarufu kama "Chicharito" ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba wa ligi daraja la kwanza Ujerumani,Bundesliga.
Tuzo hiyo ambayo ni ya tatu kwa Chicharito,28, tangu atue Ujerumani msimu mmoja uliopita imechagizwa na mabao matatu (hat-trick) aliyofunga wikendi iliyopita na kuiwezesha Bayer
Leverkusen kutoka nyuma na kuifumua Mainz 04 kwa mabao 3-2.
Chicharito ametwaa tuzo hiyo baada ya kuzoa kura 20,000 kati ya kura 28,875 zilizopigwa,akiwaacha mbali washindani wake Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund na Robert Lewandowski wa Bayern Munich.
Mchanganuo wa kura uko kama ifuatavyo
72% Chicharito
10% Robert Lewandowski
6% Christian Pulisic
12% Raphael Guerreiro
0 comments:
Post a Comment