Barcelona,Hispania.
Klabu ya Arsenal imekosa kitita cha £3m licha ya klabu ya Barcelona kutwaa ubingwa wa Ulaya mapema juzi jumamosi.
Arsenal ilitarajia kupokea bonasi ya £3m kufuatia mauzo ya mlinzi wake Thomas Vermaelen kwenda klabu ya Barcelona mwezi agosti mwaka jana.
Katika usajili huo ulioigharimu Barcelona ada ya £15m kulikuwa na kipengere ambacho kiliipa nafasi klabu ya Arsenal kupata bonasi hiyo iwapo Barcelona itatwaa ubingwa wa Ulaya ikiwa na Vermaelen kama mmoja wa wachezaji waliotia mguu uwanjani yaani kucheza japo mchezo mmoja pekee.
Mpaka Barcelona inatwaa ubingwa huo Vermaelen ameshindwa kucheza mchezo wowote licha ya mara kadhaa kuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba.Kufuatia hali hiyo klabu ya Arsenal imekosa mkwanja huo wa uhakika.
0 comments:
Post a Comment