728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 08, 2015

    DAVID LUHENDE ATUA MWADUI FC

    Timu ya soka ya Mwadui ya mkoani Shinyanga iliyopanda daraja hivi karibuni imeionyesha Yanga kuwa nayo ipo vizuri kifedha na inaweza kushindana nayo katika vita ya usajili ambayo inazidi kushika kasi hapa nchini.

    Pamoja na Luhende, Mwadui FC ilimsajili kiungo mkongwe, Nizar Khalfan kutoka Yanga.

    Ijumaa iliyopita Mwadui FC ilifanikiwa kumsajili aliyekuwa beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, David Luhende ambaye pia alikuwa akiwaniwa na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga, waliokuwa wakitaka kumrudisha kundini ili waweze kuongezea nguvu kwenye safu yao ya ulinzi.

    Inadaiwa kuwa Yanga ilikuwa imemtengea Luhende kitita cha shilingi milioni 8 ili iweze kuipata saini yake lakini Mwadau FC iliingilia kati na kuweza kuipiku klabu hiyo baada ya kumwekea mezani nyota huyo Sh milioni 10.

    “Tunamshukuru Mungu ndugu yetu kapata timu ambayo imeonyesha kumjali na kuithamini kazi yake baada ya Mwadui kuamua kumpatia mkataba wa mwaka mmoja kwa kitita cha Sh milioni 10 lakini pia atakuwa akilipwa mshahara wa shilingi milioni moja kwa mwezi.

    “Uamuzi huo wa Mwadui tumeupokea kwa mikono miwili na imeonyesha kuwa, wapo vizuri kifedha kwani wameweza kuipiku Yanga ambayo pia ilikuwa na nia ya kutaka kumrudisha kundini ila kiasi cha fedha walichokuwa wamemtengea kilikuwa ni kidogo sana,” kilisema chanzo hicho cha habari.

    Hata hivyo, Luhende amesema kuwa anajiona ni mwenye bahati na atahakikisha anaitumikia klabu hiyo kwa nguvu zake zote kwa sababu soka ndiyo kazi yake inayomfanya aishi vizuri na familia yake.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DAVID LUHENDE ATUA MWADUI FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top