Klabu ya Barcelona leo jumatatu imemtambulisha rasmi mlinzi wake mpya wa kulia Alex Vidal toka klabu ya Sevilla kwa mkataba wa miaka mitano.
Vidal 25 aliyewahi kukichezea kikosi cha U-14 cha Barcelona kabla ya kutupiwa virago amerejea
tena kwa ada ya €18m ambayo itaongezeka kwa €4m zaidi ikiwa ataonyesha kiwango kizuri.
Baada ya utambulisha huo Vidal amesema "Hii ni furaha nyingine kubwa ukiachilia kuzaliwa kwa mwanangu wa kike.Nafurahi nimerejea nyumbani.Alimaliza Vidal mzaliwa wa Catalunya.
Kusajiliwa kwa Vidal kunafungua milango kwa mlinzi Dani Alves kutimka klabuni hapo kwani amebakiza wiki tatu pekee kufikia mwisho wa mkataba wake.
0 comments:
Post a Comment