Habari na Paul Manjale
Gundogan:Mwandishi Alfredo MartÃnez ambaye yuko karibu sana na klabu ya Barcelona ametweet kuwa klabu hiyo imeachana rasmi na mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund Ilkay Gündogan 24.
Manchester United imekataa ofa toka klabu ya Valencia kwa ajili ya kumsajili mlinda mlango wake Victor Valdes ili azibe nafasi ya mlinda mlango wake No.1 Diego Alves aliyepata jeraha la goti.
Remy:Klabu ya Swansea City imeingia katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy kwa ajili ya kuongeza makali katika kikosi chake.Mbali ya Swansea vilabu vya Southampton na Crystal Palace pia viko katika mawindo ya nyota huyo toka Ufaransa. (Daily Mirror)
Austin:Klabu ya QPR imeitaka klabu ya Newcastle United kutoa kitita cha £15m kwa kweli inataka kuipata saini ya mshambuliaji wake mahiri Charlie Austin,25.
Kocha mpya wa Real Madrid Rafa Benitez ameripotiwa kuwataka nyota wawili wa klabu ya Chelsea Eden Hazard na Diego Costa kwa ajili ya kukisuka upya kikosi cha Los Blancos ambacho kinamaliza msimu bila kombe lolote.
Martial:Klabu ya Tottenham imekubali kutosa kitita cha €25 (£18.1m) kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kinda wa wa Monaco Anthony Martial 19 ambaye kiucheza kama Thierry Henry
0 comments:
Post a Comment