Habari na Paul Manjale
Mlinzi wa zamani wa vilabu ya Arsenal na Tottenham na timu ya taifa ya England Sol Campbell leo juni 8 ametangaza kuwa atagombea kiti cha umeya wa jiji la London katika uchaguzi ujao.
Campbell mwenye miaka 40 ambaye ni mzaliwa wa London amethibitisha kuwa atagombea nafasi hiyo nyeti kwa tiketi ya chama cha Conservative kuchukua nafasi ya meya wa sasa bwana Boris Johnson anayeondoka madarakani mwaka 2016.
Campbell ameongeza kuwa atakuwepo kwenye mdahalo utakaofanyika julai 4 kuchuana na wagombea wengine wa chama hicho kinachoongozwa na waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameroon.
Je,ikiwa Campbell atashinda kiti hicho na kuwa meya wa jiji hilo atakuwa imara kama alivyokuwa katika duru za soka?Ni jambo la kusubiri na kuona nini kitatokea.
0 comments:
Post a Comment