Klabu ya Liverpool imethibisha kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Burnley,Danny Ings licha ya klabu yake kushuka daraja msimu uliopita.
Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 ambaye mkataba wake unamalizika juni 30 atajiunga na Liverpool Julai 1 baada ya kukamilisha vipimo vyote vya afya.
Ings alikuwa na msimu mzuri katika timu yake akipachika jumla ya magoli 11 katika michezo 35 ya ligi kuu anakuja kuongeza makali katika klabu hiyo ilifanikiwa kupachika magoli 54 pekee katika msimu ulioisha.
Ings anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu ya Liverpool baada ya James Milner kujiunga na Majogoo hao wiki moja iliyopita kwa uhamisho huru akitokea klabu ya Manchester City.
Ujio wa Ings huenda ukawa unamaanisha ni mwisho wa washambuliaji Mario Balotelli na Rickie Lambert ambao kwa ujumla wao wamepachika jumla ya magoli matatu (3) pekee.
0 comments:
Post a Comment