Yaounde,Cameroon.
HALI ya afya ya nahodha wa zamani wa Cameroon,Rigobert Song Bahanag,imeripotiwa kuanza kutengemaa hii ni baada ya kuzinduka na kuanza kupumua bila ya msaada wa mashine ya Okisijeni.
Mapema siku ya Jumapili,Song,mwenye umri wa miaka 40 alipoteza fahamu baada ya kupatwa na shambulio baya la ugonjwa wa kiharusi hali iliyofanya akimbizwe katika kituo cha afya cha wagonjwa wa dharura cha Messa akiwa hajitambui.
Taarifa kutoka kituo cha afya cha Messa zinasema nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Metz,Lens,Liverpool,Westham United na Galatasaray alizinduka jana jioni na tayari amesafirishwa kwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment