728x90 AdSpace

Wednesday, October 05, 2016

HAWA HAPA 10 WANAOWANIA TUZO YA KOCHA BORA,MCHEZAJI BORA WA MWEZI 9 LIGI KUU ENGLAND


London,Uingereza.

BAADA ya mwezi Septemba kwisha,chama cha soka England,FA,kimetoa majina ya makocha watano,wachezaji watano wanaowanoa tuzo ya kocha/mchezaji bora wa mwezi Septemba.Washindi watatangazwa Octoba 10.

KOCHA BORA WA MWEZI

Pep Guardiola (Manchester City),Jurgen Klopp (Liverpool),Alan Pardew (Crystal Palace) na Mauricio Pochettino (Tottenham Hotspur).Makocha wote watano wameshinda michezo mitatu mwezi Septemba.

MCHEZAJI BORA WA MWEZI

 

Kevin De Bruyne (Manchester City)Amefunga mabao mawili na kutengeneza/assist mawili

Adam Lallana (Liverpool) Amefunga mabao mawili na kutengeneza/assist mawili. Bao dhidi ya Leceister City limeingia katika kinyang'anyiro cha kusaka bao bora la mwezi Septemba maarufu kama Carling Goal of the Month award.

Romelu Lukaku (Everton).Amehusika katika upatikanaji wa mabao mengi zaidi kuliko wote mwezi Septemba.Alifunga mabao matatu ( hat-trick) Sunderland.Alifunga bao moja dhidi ya Crystal Palace.Pia katika mchezo dhidi ya Middlesbrough alifunga bao moja na kupika/kutengeneza moja.

Son Heung-min (Tottenham Hotspur).Amefunga mabao manne.Mawili dhidi ya Stoke City na mawili dhidi ya Middlesbrough.Bao lake la pili dhidi ya Stoke City limeingia katika kinyang'anyiro cha kusaka bao bora la mwezi Septemba maarufu kama Carling Goal of the Month award.

Theo Walcott (Arsenal).Amefunga mabao mawili na kuiwezesha Arsenal kushinda michezo mitatu mwezi Septemba.


WANAOWANIA TUZO YA BAO BORA LA MWEZI SEPTEMBA

Adam Lallana (LIVERPOOL v Leicester City) 10 September

Callum Wilson (AFC BOURNEMOUTH v West

Bromwich Albion) 10 September

Steven Defour (BURNLEY v Hull City) 10

September

Son Heung-min (Stoke City v SPURS) 10 September

Troy Deeney (West Ham v WATFORD) 10 September

Jordan Henderson (Chelsea v LIVERPOOL) 16 September

Granit Xhaka (Hull City v ARSENAL) 17 September

Demarai Gray (Manchester United v

LEICESTER CITY) 24 September


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: HAWA HAPA 10 WANAOWANIA TUZO YA KOCHA BORA,MCHEZAJI BORA WA MWEZI 9 LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown