Nice,Ufaransa.
MARIO BALOTELLI ameendelea kuionyesha klabu yake mpya ya OGC Nice ya Ufaransa kuwa haikukosea kumsajili mwishoni mwa mwezi Agosti hii ni baada ya Jumapili usiku kuifungia bao pili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Lorient.
Bao hilo la dakika ya 87 limemfanya Balotelli awe ameifungia OGC Nice mabao sita katika michezo mitatu ya ligi na kuipeleka klabu hiyo kileleni kabisa mwa msimamo wa ligi. Bao la kwanza la OGC Nice limefungwa na Ricardo Pereira huku lile la Lorient likifungwa na Benjamin Moukandjo.
Alimwa kadi nyekundu!!
Mario Balotelli alianza kulimwa kadi ya njano dakika ya 87 kwa kosa la kuvua jezi wakati akishangilia bao alilofunga ambalo lilikuwa na ushindi kwa OGC Nice.
Dakika sita baadae yaani dakika ya 93 alilimwa kadi nyekundu baada ya kuleteana ubabe na beki wa Lorient,Steve Moreira.Hii ina maana Balotelli ataukosa mchezo ujao dhidi ya Olympique Lyon.
0 comments:
Post a Comment