728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 13, 2015

    USAJILI:DE GEA AIGEUKA UNITED,CECH ATISHIWA MAISHA CHELSEA

    Mikel:Kiungo wa Chelsea John Obi-Mikel huenda akaondoka klabuni hapo na kutua Uturuki kukipiga katika klabu ya Fenerbache.Habari toka Uturuki zinadai mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Fenerbache Giuliano Terraneo ameelekea London kwa ajili ya mazungumzo ya kina juu ya uhamisho wa nyota huyo toka Nigeria.

    Song:Kocha wa klabu ya Chelsea Mreno Jose Mourinho anafikiria kumsajili kiungo wa klabu ya Barcelona Alex Song kwa ajili ya kuongeza nguvu na kutoa changamoto kwa kiungo Nemanja Matic.Mourinho yuko tayari kutoa kitita cha £6m ili kumsajili saa huyo wa zamani wa Arsenal.

    Martinez:Raisi wa klabu ya Fc Porto Pinto Da Costa amesema mshambuliaji wa klabu hiyo Jackson Martnez 28 amechagua kujiunga na klabu bingwa ya zamani ya Italia Ac Milan na mpango wa kutua England kuchezea Arsenal ama Liverpool.

    Ghoulam:Vilabu vya Chelsea na Manchester City vimeripotiwa kugombea saini ya mlinzi wa kushoto wa klabu ya Napoli Mserbia Faouzi Ghoulam.Napoli iko tayari kumuuza mlinzi huyo mahiri ikiwa itapokea kitita cha €15m.

    Richards:Mlinzi aliyetemwa na klabu ya Manchester City Micah Richard amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Sunderland na badala yake atatua katika klabu ya Aston Villa.

    Edin Dzeko:Klabu ya Arsenal kupitia kwa kocha wake mkuu Arsene Wenger imeripotiwa kumuweka katika orodha ya nyota inaowataka mshambuliaji wa Manchester City Mbosnia Edin Dzeko,28.Dzeko aliyecheza michezo 11 ya ligi kuu na kufunga magoli 4 anaonwa kama mtu sahihi wa kutoa upinzani kwa Mfaransa Olivier Giroud.

    Cech:Uhamisho wa mlinda mlango Peter Cech 33 huenda ukawa wa mashaka baada ya shabiki mmoja wa Chelsea kumtishia nyota huyo kuwa endapo atatua Arsenal basi ajiandae kuitwa "Msaliti" na kufanyiwa yote kama anayofanyiwa Robin Van Persie na mashabiki wa Arsenal.

    De Gea:Mlinda mlango David De Gea ameripotiwa kujiandaa kutuma barua kwa ajili ya kuiomba na kuishinikiza klabu yake ya Manchester United imuachie atimize ndoto ya kutua katika klabu ya nyumbani kwao Hispania ya Real Madrid.Madrid imeandaa kitita cha £25m ili kumnasa nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:DE GEA AIGEUKA UNITED,CECH ATISHIWA MAISHA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top