Cardiff,Wales
Gareth Bale ameendelea kudhihirisha kuwa yeye ni mkali baada ya hapo jana usiku kuipatia pointi 3 timu yake ya taifa ya Wales mbele ya Ubelgiji katika kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya michuamo ijayo ya Euro 2016.
Akicheza mbele ya mashabiki lukuki waliofurika katika dimba la Cardiff,Bale aliuwahi mpira wa kichwa uliorudishwa nyuma kwa makosa na kiungo wa Ubelgiji Radja Nainggola na kumchambua mlinda mlango Thibaut Courtois na kufunga bao lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Kufuatia ushindi huo Wales imaongoza kundi B ikiwa na jumla ya alama 14,Ubelgiji nafasi ya pili ikiwa na alama 11 huku Bosnia ikiwa na alama 9.Timu mbili ndiyo zitakazofuzu kuingia katika michuano hiyo itakayopigwa nchini Ufaransa hapo mwakani
Matokeo mengine:
Latvia 0-2 Uholanzi (Georginio Wijnaldum,Luciano Narsingh)
Iceland 2-1 Czech Republic (Aron Gunnarsson,Kolbeinn Sigtho)
Croatia 1-1 Italia (Mandzukic,Antonio Candreva)
0 comments:
Post a Comment