728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 07, 2015

    USAJILI:CITY KUHAMIA KWA BENDER IKIMSHINDWA POGBA,JUVENTUS YAJA TENA KWA VAN PERSIE

    Habari na Paul Manjale

    Llorente:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kumpigia mahesabu mshambuliaji anayesota benchi katika klabu ya Juventus Fernando Llorente (30) ambaye anaweza kupatikana kwa bei chee ya £5m.

    Bielsa:Kocha wa klabu ya Marseille ya Ufaransa Marcelo Bielsa ameonyesha nia ya dhati baada ya kuwaambia jamaa zake wa karibu kuwa anavutiwa na kibarua cha kuinoa klabu ya Westham ya England.

    Martinez:Ndoto za klabu ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Fc Porto Mcolombia Jackson Martinez (28) zimeendelea kuwa hai baada ya klabu hiyo ya Ureno kukataa ofa ambayo haijawekwa wazi toka klabu ya Atletico MadrMadrid.

    Van Persie:Klabu ya Juventus imeripotiwa kuandaa kitita cha £5m kwa ajili ya kumsajili mshambulia wa Manchester United Robin Van Persie (31).Juventus inarejea tena kumtaka Van Persie baada ya kushindwa kumsajili miaka minne iliyopita wakati akiwa Arsenal.

    Anderson:Kocha wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal ameripotiwa kuwa tayari kuandaa kitita cha £30m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Lazio Felipe Anderson ili kuimarisha safu kikosi chake kwa ajili ya michuano ijayo ya Ulaya.

    Song:Klabu ya Southampton imeripotiwa huenda ikafikiria kumsajili kiungo wa Fc Barcelona Alex Song ikiwa kiungo wake Mfaransa Morgan Schneiderlin ataamua kuondoka klabuni hapo St Marys.Song ametengewa £8m.

    Bender:Kiungo Lars Bender wa klabu ya Bayer Leverkusen ameanza kutajwa katika klabu ya Manchester City kama mbadala ikiwa klabu hiyo itashindwa kumsajili kiungo Paul Pogba toka Juventus mwenye thamani ya £70m.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:CITY KUHAMIA KWA BENDER IKIMSHINDWA POGBA,JUVENTUS YAJA TENA KWA VAN PERSIE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top