Kocha mpya wa timu ya Togo Tom Saintfiet amemshtumu nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor kwa ukosefu wa nidhamu baada ya mshambuliaji huyo wa Tottenham kushindwa kujiunga na kikosi hicho kwa wakati ufaao kwa mechi ya ufunguzi ya kufuzu kwa kombe la Afrika wikendi ijayo.
''Nilimuona siku ya jumatano na Ijumaa lakini hayuko hotelini'',Saintfiet aliviambia vyombo vya habari mjini Lome siku ya ijumaa.
Kocha huyo kutoka Ubelgiji alikuwa akizungumza kabla ya kuondoka kuelekea Togo ili kushiriki katika mechi ya kirafiki na Ghana siku ya jumatatu.
''Ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa timu hii lakini siwezi kushirikiana nao iwapo hawako katika timu,ni lazima wawe na nidhamu kama wengine''.
Kikosi cha kitaifa cha Togo kitacheza na Liberia mjini Lome siku ya jumapili katika mechi za kundi A .
Klabu ya Adebayor Tottenham ilimpatia likizo mara mbili msimu huu ili kurudi nyumbani na kusuluhisha maswala ya kibinafsi ambayo mshambuliaji huyo amelalamikia katika mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment