Habari na Paul Manjale
Kombe la dunia la wanawake lilianza kutimua vumbi lake jana nchini Canada.
Katika mchezo wa ufunguzi wenyeji Canada waliifunga China goli 1-0 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa kiufundi na nahodha wake Christine Sinclair baada ya mlinzi wa China Zhao Rong kumfanyia madhani Adriana Leon wa Canada.
Kutoka kundi B:Timu ya taifa ya Ujerumani imetoa onyo baada ya kuwatandika wawakilishi wa Afrika timu ya Ivory Coast kwa jumla ya magoli 10-0 katika mchezo ukiopigwa katika dimba la Lansdowne,Ottawa.
Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Celia Sasic 3', 14', 31'; Anja Mittag 29', 35', 64'; Simone Laudehr 71'; Sara
Daebritz 75'; Melanie Behringer 79';Alexandra Popp 85'
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Norway iliibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Thailand.
0 comments:
Post a Comment