728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 08, 2015

    REKODI ZOTE KALI ZA LIGI YA MABINGWA ZIKO HAPA

    Imeandaliwa na Paul Manjale

    Ikiwa ni miaka 23 imepita tangu michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kuingia katika mfumo mpya mwaka 1992 zifuatazo ni rekodi kali za michuano hiyo.

    GOLI LA MAPEMA ZAIDI LA LIGI YA MABINGWA ULAYA.

    Unamkumbuka Mdachi Roy Makaay?Nyota wa zamani wa vilabu vya Bayern Munich na Derpotivo la Coruna,anashikiria rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi baada ya kuifunga Real Madrid akiwa na klabu ya Bayern Munich hiyo ikiwa ni mwaka 2007.

    Makaay alifunga goli hilo sekunde ya  10 tu tangu kuanza kwa mchezo.Mpaka mwisho Bayern 2-1 Madrid.

    ORODHA KAMILI HII HAPA..

    1. Roy Makaay | 10.12 | 2007
    2. Jonas | 10.96 | 2011
    3. Gilberto Silva | 20.07| 2002
    4. Del Piero | 20.12| 1997
    5. Clarence Seedorf |21.06|2005
    6. Pato | 24.97| 2011
    7.Marek Kincl | 25.20| 2005
    8. Dejan Stankovic | 25.54| 2011
    9. Mariano Bombarda | 28.21| 1999
    10. Alexis Alexoudis | 28.46| 1995

    HAT-TRIK YA MAPEMA ZAIDI KUFUNGWA

    Nyota wa zamani wa Lyon Batefimbi Gomis alitumia dakika 7 pekee kufunga magoli matatu hii ni katika mechi dhidi ya Dinamo Zagreb akiivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mshambuliaji wa Blackburn Rovers Mike Newell baada ya kufunga hat-trik dani ya dakika 9 dhidi ya Rosenborg mwaka 1995.Lyon ilishinda 7-1.

    BARCELONA v JUVENTUS

    Barcelona imeshinda fainali nne kati ya tano ilizocheza.Ilianza kwa kupoteza ile ya mwaka 1994 kisha ikashinda nyingine zote ambazo ni zile za 2006 , 2009 , 2011 na 2015.

    Wakati Barcelona wao wakifurahia rekodi hiyo nzuri wenzao Juventus hali siyo shwari kwani wamepoteza jumla ya fainali nne wakianzia ile ya mwaka 1997 , 1998 , 2003 na kisha 2015.

    WAFUNGAJI BORA WALIOWAHI KUFUNGANA..

    1999/2000 washambuliaji watatu walifungana baada ya wote kufunga magoli 10 kila mmoja na tuzo kwenda kwa wote.Washambuliaji hao ni Mário Jardel (Fc Porto),Rivaldo (Barcelona) na  Raúl González (Real Madrid) magoli 10

    2014/2015
    Ronaldo,Neymar na Messi wamefungana baada ya kila mmoja kufunga magoli 10.Ronaldo na Neymar wamefunga magoli hayo baada ya kucheza michezo 12 huku Messi akifikisha idadi hiyo baada ya kucheza michezo 13.

    GOLI LA MAPEMA ZAIDI LA FAINALI....

    Goli la mapema zaidi la mchezo wa fainali lilifungwa na mlinzi wa klabu ya Ac Milan Paolo Maldini mwaka 2005 katika dakika ya 1 ya tu  mchezo wa fainali dhidi ya Liverpool FC,anafuatia Gaizka Mendieta katika nafasi ya pili baada ya kuifungia Valencia goli dakika ya 3 dhidi ya klabu ya Bayern Munich mwaka 2001.

    KADI NYEKUNDU YA MAPEMA ZAIDI

    Mlinzi wa klabu ya Shakhtar Donetsk  Olexandr Kucher anashikilia rekodi ya kupewa kadi nyekundu ya mapema zaidi baada ya kupewa dakika 3 tu tangu mchezo uanze.Hii ilikuwa ni mwaka huu baada ya mlinzi huyo kumfanyia madhambi Mario Gotze wa Bayern Munich na mwamuzi Willie Collum toka Scotland kuamuru ipigwe penati.

    ALVARO MORATTA
    Mshambuliaji huyu kinda aliyejiunga na Juventus msimu huu anakuwa mchezaji wa kwanza kuzifunga timu za nyumbani kwao akiwa na klabu ya taifa jingine.

    Moratta alianza kuifunga klabu yake iliyomkuza ya Real Madrid katika michezo miwili ya nusu fainali kabla ya kuhitimisha na goli la kufutia machozi dhidi ya Barcelona katika mchezo wa fainali uliopigwa huko Olympic,Berlin Ujerumani.

    XAVI HERNANDEZ

    Kiungo na nahodha Xavi Hernandez ameweka rekodi baada ya kucheza jumla ya michezo 151 ya ligi ya mabingwa akimzidi mlinda mlango wa Real Madrid Iker Cassillas kwa mchezo mmoja.Hata hivyo rekodi hiyo inatazamiwa kuvunjwa mapema kwani sasa ni rasmi Xavi ameachana na soka la Ulaya huku Casillas yeye akiwa bado ni chaguo la kwanza katika kikosi cha Real Madrid.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REKODI ZOTE KALI ZA LIGI YA MABINGWA ZIKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top