Manchester, England.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka Paul Scholes amesema mlinzi wa klabu hiyo Phil Jones hana akili ya kutosha kuimudu nafasi ya ulinzi wa kati katika klabu hiyo na timu ya taifa ya England.
Akiongea leo na kunukuliwa na mtandao huu wa Soka Extra,Scholes amesema
"Jones hana akili ya kutosha kucheza nafasi hiyo ya ulinzi.Mara nyingi anapokutana na washambuliaji wengi akili za kutosha huwa anapitika kirahisi sana.
"Nadhani anapaswa aendelee kucheza nafasi yake ya ulinzi wa kulia ambayo amekuwa akiicheza na kuimudu kutokana na kuwa na nguvu na uwezo wa kutosha lakini siyo kati.
Jones ambaye leo alishuka dimbani na kikosi cha England na kutoka 0-0 tangu atue Manchester United amecheza katika nafasi za ulinzi wa kati,kulia na kiungo cha ulinzi.
0 comments:
Post a Comment