Barcelona,Hispania.
Raisi wa klabu bingwa ya Ulaya FC Barcelona Josep Bartomeu amekiri kuwa timu timu yake inaisaka kwa udi na uvumba saini ya kiungo nyota wa klabu ya Juventus Paul Pogba.
Akizungumza na mtandao wa Telefoot leo hii baada ya klabu yake kutwaa ubingwa wa Ulaya hapo jana Bartomeu amesema
"Pogba ni chaguo letu namba moja katika kipindi hiki cha usajili lakini siwezi kuzungumza mengi kwa sasa kutokana na kuwa bado tunatumikia adhabu ya kutofanya usajili wowote mpaka hapo januari mwakani."Alimaliza Josep Bartomeu
Iwapo Barcelona itafanikiwa kumsajili Pogba basi nyota huyo atalazimika kukaa nje ya uwanja na kufanya mazoezi na kikosi cha vijana mpaka mwezi januari.
0 comments:
Post a Comment