Habari na Paul Manjale
Cech:Mlinda mlango wa Chelsea Peter Cech leo jumatatu atakutana na viongozi wa klabu hiyo ili kujua hatima yake
klabuni hapo.Cech anataka kuhamia Arsenal kwa ada ya £11m lakini uongozi wa Chelsea unataka kumuuza katika klabu ya PSG.
Dost:Klabu ya Newcastle iko mbio kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari wa Wolfsburg Bas Dost (26) kwa ada ya £9m.Dost atasaini mkataba wa miaka minne,amefunga magoli 16 katika ligi ya Bungesliga na kuiwezesha Wolfsburg kutwaa ubingwa wa kombe la ligi (DFB).
Anderson:Kocha wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal ameripotiwa kutenga kitita cha £30m kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa Lazio Mbrazil Felipe Anderson kwa ajili ya kukipa makali kikosi chake.
Richards:Mlinzi wa klabu ya Manchester City Micah Richards 26 wiki hii anatarajiwa kupima afya yake kabla ya kumwaga wino wa kuichezea klabu ya Aston Villa.
Sterling:Klabu ya Manchester City ina matumaini ya kumsajili winga wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling kwa ada ambayo iko chini ya £50m inayotakiwa na miamba hiyo ya Anfield.
Mourinho:Kocha wa Chelsea Jose Mourinho yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuifundisha miamba hiyo ya ligi kuu ya England.Mkataba huo mpya ambao utakuwa wa miaka 4 utamuwezesha kocha huyo kuvuna kitita cha £30m.
Falcao:Mshambuliaji Radamel Falcao ameripotiwa kufikia makubaliano binafsi ya kujiunga na klabu ya Chelsea kilichobaki ni Chelsea kufanya mazungumzo na klabu yake ya Monaco ili usajili huo ukamilike.
0 comments:
Post a Comment