728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 15, 2015

    YANGA YAFUNGUKA KUHUSIANA NA SUALA LA OKWI

    Uongozi wa Yanga umetangaza kuwa, kamwe haitamsajili profesheno yeyote aliyewahi au anaiyechezea timu za Ligi Kuu Bara na kwamba ni upuuzi mkubwa kuhusishwa na suala la kumrejesha Emmanuel Okwi kutoka Simba.
    Emanuel Okwi

    Hiyo ni siku chache tangu ivumi
    shwe kuwa Okwi amesajiliwa Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

    Ukiachana na Okwi, baadhi ya wachezaji wa kimataifa wanaotajwa kwenye usajili wa timu hiyo ni Waivory Coast Pascal Wawa na Kipre Tchetche.

    Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alisema kuwa ili kuepukana na matatizo, wameona wachukue maamuzi hayo ya kutosajili wachezaji wa kimataifa wanaozichezea au waliowahi kuzichezea klabu za hapa nchini.

    Tiboroha alisema wanaamini wapo wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kuichezea Yanga ambao wamepanga kuwaleta kutoka Nigeria,Ghana, Zimbabwe na Sierra Leone ambao wakati wowote watatua nchini.

    “Kamwe hautakuja kusikia Yanga imemsajili mchezaji wa kimataifa aliyewahi au anayeichezea klabu yoyote inayoshiriki ligi kuu nchini hapa.
    “Kama wachezaji wapo wengi
    tu kutoka kwenye mataifa mbalimbali, ndiyo maana tumepanga kuwaleta Waghana, Mzimbabwe,Mnigeria na Msierra Leone ambao watakuja kwa ajili ya kuichezea Yanga.

    “Hiyo ni moja ya mikakati tuliyoipanga Yanga katika usajili wetu wa msimu huu na miaka ijayo, labda uongozi mpya uingie lakini siyo huu wetu,”alisema Tiboroha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAFUNGUKA KUHUSIANA NA SUALA LA OKWI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top