728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 15, 2015

    TFF YAKWAMISHA HESABU ZA YANGA



    Yanga  bado inapiga hesabu kali kukamilisha usajili wao kwa wachezaji wa Kimataifa, lakini sasa yameibuka mambo mapya matatu katika ujio wa wachezaji hao.

    Taarifa kutoka n
    dani ya uongozi wa Yanga kupitia kamati yake ya usajili, klabu hiyo tayari ina uhakika wa kupata wachezaji watatu kutoka Ghana, kati yao viungo wawili na beki ambaye nafasi yake ni siri kubwa.

    Katika mpango huo Yanga imeonekana kuumiza kichwa baada ya kupata taarifa za awali kuwa TFF wanaweza kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kufikia saba tofauti na maombi na ya klabu za Ligi Kuu kutaka wachezaji 10.

    Wakati hali ikiwa hivyo upande huo wa TFF, pia Yanga imekosa maamuzi ya haraka kufuatia mpango wa kurudi kwa muda kwa kiungo wao Mbrazil Andrey Coutinho na mshambuliaji Kpah Sherman waliokuwa katika mpango wa kutemwa na kutafutiwa timu nyingine.

    Kurudi kwa Coutinho na Sherman raia wa Liberia ni ugumu mwingine kwa Yanga na sasa mabosi wa timu hiyo wanapiga hesabu kali kwa kuangalia kuwapunguza Waghana wao.

    Tayari Yanga kabla ya kuachwa Coutinho na Sherman imekamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni wakiwamo beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe.

    Akili ya Yanga ni kwamba endapo TFF itaruhusu wachezaji saba tu nafasi hizo mbili za nyongeza zitumiwe kujazwa kwa mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Lansana Kamara huku wakitaka kufanya juu chini kulazimisha uhamisho wa Coutinho kumpisha kiungo mmoja wa pembeni Mghana.

    “Bado hatujaamua tupo njia panda kama TFF watabadili mipango ambayo klabu tulikubaliana, hii inatupa shida kidogo kuna uwezekano baadhi ya wachezaji wakasubiri mpaka dirisha dogo la usajili,” alisema bosi mmoja wa usajili.

    Alisema Waghana ni watu wa kazi japo baadhi wana mikataba huko walipo na Yanga imepanga kumpa miezi sita Mliberia Sherman na akisuasua wanamtema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF YAKWAMISHA HESABU ZA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top