Campbell:Klabu ya Fenerbahce imeripotiwa kufikia makubaliano na klabu ya Arsenal juu ya kumsajili mshambuliaji kinda Joel
Campbell.Arsenal inataka kumuuza Campbell pamoja na washambuliaji Lukas Podolski na Yaya Sanogo ili kupata pesa za kusajili washambuliaji wapya.
Austin:Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amedaiwa kuanza kujipanga kumsajili mshambuliaji wa QPR Charlie Austin (25) baada ya kukoshwa na kiwango alichokionyesha msimu ulioisha.Mourinho anasaka mshambuliaji mpya ili kuongeza ngumu katika safu yake ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Didier Drogba.
Falcao:Mshambuliaji Radamel Falcao ameripotiwa kufikiria kuachana na mpango wa kutua klabu ya Chelsea na badala yake atatua klabu ya Liverpool.Falcao anaamini Liverpool itampa muda mwingi wa kucheza na kurejesha makali yake tofauti na Chelsea ambako ushindani wa namba ni mkubwa.
Kondogbia:Baada ya fununu za muda mrefu juu ya kutakiwa kwa nyota wake wa kiungo hatimaye klabu ya Monaco imetangaza bei ya Geoffrey Kondogbia.Monaco imesema Kondogbia 22 ana thamani ya £24.6m hii ni baada ya kuipiga chini ofa ya £18m toka klabu ya Arsenal mwishoni mwa wiki iliyopita.
Pellegrini:Klabu ya Manchester City imeripotiwa kuwa bado inahitaji huduma ya kocha wake wa sasa Manuel Pellegrini licha ya kumaliza msimu uliopita bila taji lolote.Pellegrini bado ataendelea kuwanoa matajiri hao wa ligi ya EPL kwa msimu ujao.
Gotze:Klabu ya Bayern Munich imeripotiwa kumuweka sokoni kiungo wake Mario Gotze baada ya kutoridhishwa na mchango wa nyota huyo wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund.Miongoni mwa vilabu vinavyoitaka hudumu ya nyota huyo ni Manchester United, Arsenal na Chelsea
0 comments:
Post a Comment